Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

TPHPA ni nini?

Historia ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticides Research Institute - TPRI) ilianza mwaka1945chini ya ofisi ya utawala wa kikoloni wa Kiingereza.Kulikuwa na kikundi cha wataalamu huko London, Uingereza kilichojishughulisha na unyunyiziaji wa viuatilifu vilivyotengenezwa kiwandani kwa ajili ya kudhibiti visumbufu wa ukanda wa tropiki. Kikundi hiki kilianzia shughuli zake Entebe nchini Uganda wakiwa wamejikita katika utafiti wa ndorobo na mbu.  Mnamo mwaka 1950 kikundi hiki kilihamia Arusha bado kikiwa chini ya utawala wa kikoloni na kuanzisha kituo kilichoitwa “Colonial Insecticides Research Unit (CIRU)”. Mwaka 1962 CIRU iliunganishwa katika shughuli za kitafiti za Shirika la Pamoja la Nchi za Afrika ya Mashariki (East African Common Services Organisation – EACSO). Baada ya muda mfupi shughuli hizi zilipanuka na kuongezeka kutoka kusimamia utafiti wa viuadudu hadi viuagugu, vizuiakuvu, na viuakonokono waenezao kichocho. Kwa wakati huo katika nchi za Afrika Mashariki watafiti walikuwa wachache kwenye nyanja za biolojia ya wadudu na mimea. Mwaka 1967 Jumuiya ya Afrika Mashariki iliundwa na shughuli za EACSO zikachukuliwa na Shirika la Udhibiti wa Viuatilifu la Afrika Mashariki (East African Pesticides Control Organization - EAPCO). Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977, na Serikali ya Tanzania ikaunda Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticides Research Institute - TPRI) kupitia Sheria Na. 18 ya 1979. Lengo la Sheria hii ambayo bado ipo na inatumika ni “Kuunda Taasisi ya Utafiti ywa Viuatilifu Katika Ukanda wa Kitropiki, ili kuipa Mamlaka ya kudhibiti viuatilifu, pamoja na kuruhusu shughuli nyingine za kitaasisi sawa na lengo la uanzishwaji wake” (“to establish the Tropical Pesticides Research Institute, to provide for the research and pesticides control, the functions of the Institute and for the matters connected with and incidental to the establishment of the Institute”).