Kanda ya Kusini
Kanda ya Kusini
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania Kanda ya Kusini ipo Kusini mwa Tanzania ambayo inahudumia Mikoa mitatu (3); Mtwara, Lindi na Ruvuma. Ofisi za Kanda zipo katika Mkoa wa Mtwara. Kazi kubwa ya kanda ni kusimamia/kudhibiti Afya ya Mimea na viuatilifu katika Mikoa tajwa hapo juu.
Majukumu ya kanda ya Kusini:
- Ukaguzi wa shehena za Mazao, Mimea Viuatilifu na bidhaa zingine za Kilimo zinazodhibitiwa na mamlaka zinazoingia na kutoka Nchini.
- Kutoa vyeti vya usafi kwa mazao, mimea na bidhaa zitokanazo na mimea zinazosafirishwa kwenda nje ya Nchi
- Ukaguzi wa maduka ya viuatilifu kwa wadau wa viuatilifu pamoja na kuwezesha usajili mpya kwa wafanyabiashara wa viuatilifu.
- Ukaguzi wa maghala ya mazao na viuatilifu.
- Kutoa mafunzo ya utambuzi na udhibiti wa visumbufu vya Mimea kwa mazao
- Kutoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu.
- Ukaguzi wa mashamba maalumu ya mazao yanayosafirishwa kwenda nje ya Nchi.
- Ukaguzi wa meli zinazoingia Nchini.
- Uchunguzi na utabiri wa viashiria vya awali vya visumbufu vya mlipuko (Panya na Viwavi jeshi) katika maeneo yanayokabiliwa na visumbufu hivyo.
- Vituo vya Ukaguzi vilivyopo Kanda ya Kusini:
- Bandari (Mtwara, Lindi, Kilwa- Lindi na Mbambabay- Ruvuma)
- Vituo vya mipakani (Mtambaswala- Mtwara, Kilambo- Mtwara, Chihanga- Mtwara na Mkenda- Ruvuma)
- Viwanja vya Ndege (Mtwara na Songea)
- Ofisi za Posta (Mtwara, Lindi and Ruvuma)
Anuani ya Posta
TPHPA Kanda ya Kusini,
S.L.P 560,
Mtwara.
Barua pepe