Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

TPHPA YASAINI HATI YA MASHIRIKIANO NA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA (TPHPA)

Imewekwa: 27 Aug, 2025
TPHPA YASAINI HATI YA MASHIRIKIANO NA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA (TPHPA)

ARUSHA, 27 AGOSTI 2025 – Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo wamesaini hati ya makubaliano ya mashirikiano (MoU) katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TPHPA, jijini Arusha. Hafla hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa menejimenti wa taasisi hizo pamoja na wanasheria waliokuwa sehemu ya maandalizi na ushauri wa makubaliano hayo.

Akizungumza wakati wa utiaji saini, Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Prof. Joseph Ndunguru, alisisitiza kuwa ushirikiano huo ni hatua muhimu ya kuimarisha uwezo wa kitaasisi na kitaalamu. Amefafanua kuwa makubaliano hayo yatajikita katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuandaa moduli za mafunzo kwa wakulima juu ya matumizi salama ya viuatilifu, kuongeza ujuzi wa watumishi wa TPHPA katika mifumo ya kifedha na sheria za manunuzi, kufanya tafiti za pamoja, na kushirikiana katika miradi ya mafunzo na utafiti.

Prof. Ndunguru pia alibainisha kuwa mashirikiano haya yanatarajiwa kuwa chachu ya mafanikio katika kutekeleza majukumu ya taasisi zote mbili, sambamba na kujenga mazingira salama kwa afya ya mimea, binadamu, wanyama na mazingira. Kwa upande wake, Prof. William A. Pallangyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, alisema kwamba ushirikiano huo “umekuja kana kwamba umechelewa,” hivyo taasisi hizo sasa zitausimamia kwa karibu na kuanza utekelezaji mara moja ili kuhakikisha matokeo chanya yanapatikana kwa haraka.