Kanda ya Magharibi
Kanda ya Magharibi
TPHPA Kanda ya Magharibi iko upande wa magharibi wa Tanzania na inahusisha mikoa ya minne (4) ambayo ni Tabora, Kigoma, Rukwa, na Katavi, Tabora ikiwa ni Makao Makuu ya ukanda huo na Ofisi zipo ndani ya jengo la Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (TUWASA). Ina mipaka mitatu ya nchi kavu na Bandari sita, ambazo zote zinatumika kuingiza na kusafirisha Vipando/mimea na mazao ya Kilimo.
KAZI ZINAZOFANYWA NA OFISI ZA KANDA
- Ukaguzi wa maduka na maghala ya kuuza na kuhifadhi viuatilifu.
- Kukusanya sampuli za viuatilifu mimea na kupeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi.
- Kutoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu kwa wakulima, wafanyabiashara na wadau mbalimbali.
- Udhibiti wa magonjwa ya milipuko, wadudu waharibifu wa mazao kama vile viwavijeshi, nzi wa matunda, nzige na kwelea kwelea.
- Ukaguzi wa viwanda vinavyotengeneza, makapuni yanayosambaza viuatilifu na vinyunyizi kwa mujibu wa sheria ya Afya ya Mimea na kanuni zake.
- Kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu kuhusu udhibiti wa visumbufu vya mazao na viuatilifu.
Mawasiliano:
Contact:
P.O. Box 2034 GONGONI TABORA
Email; tabora@tphpa.go.tz
Phone: 0655075810