Kanda ya Kati
Kanda ya Kati
Kanda ya Kati imeundwa na Mikoa miwili (2) ambayo ni Dodoma na Singida .Ofisi zipo Jiji la Dodoma, Kata ya Kilima, Mkabala na Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, barabara ya Askari.
KAZI ZINAZOFANYWA NA OFISI ZA KANDA
- Ukaguzi wa maduka na maghala ya kuuza na kuhifadhi viuatilifu.
- Kukusanya sampuli za viuatilifu mimea na kupeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi.
- Kutoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu kwa wakulima, wafanyabiashara na wadau mbalimbali.
- Udhibiti wa magonjwa ya milipuko, wadudu waharibifu wa mazao kama vile viwavijeshi, nzi wa matunda, nzige na kwelea kwelea.
- Ukaguzi wa viwanda vinavyotengeneza, makapuni yanayosambaza viuatilifu na vinyunyizi kwa mujibu wa sheria ya Afya ya Mimea na kanuni zake.
- Kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu kuhusu udhibiti wa visumbufu vya mazao na viuatilifu.
Mawasiliano:
S.L.P 2177
Email: Dodoma@tphpa.go.tz
Simu: 0754 091784, 0652 837134