Kanda ya Ziwa
Kanda ya Ziwa
Tunafurahi kukukaribisha rasmi katika familia ya TPHPA Kanda ya Ziwa. Kanda hii inahudumia Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Simiyu, na Kagera. Pia ina jukumu muhimu la kulinda afya ya mimea, mazingira, na kilimo katika maeneo haya, ili kuhakikisha usalama wa chakula na kuimarisha maisha ya wakulima na wananchi kiujumla.
2. Majukumu Muhimu ya TPHPA Kanda Ya Ziwa.
- Udhibiti visumbufu vya mlipuko kama kwelea kwelea na panya. Vilevile, tunafanya udhibiti wa viwavi jeshi na nzi wa matunda, ambavyo ni tishio kubwa kwa mazao ya kilimo katika kanda ya ziwa.
- Kutoa elimu kwa wakulima wadogo kuhusu uthibiti husishi wa visumbufu na magonjwa ya mimea (IPM), mbinu hizi zinasaidia kuongezeka kwa ubora wa chakula, usalama wa mazingira na afya ya binadamu.
- Ukaguzi wa mazao na mimea kupitia vituo vya mipakani, viwanja vya ndege na bandari ili kudhibiti visumbufu hatarishi vya mazao ndani na nje ya nchi.
- Utoaji wa vyeti vya usafi (Phytosanitary certificates) na kibali cha kuingiza mazao na mimea (PIP) yaliyokidhi vigezo na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.
- Kufanya ukaguzi na usajili wa Maduka ya Viuatilifu ili kuhakikisha ubora, sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa biashara ya viuatilifu zinafuatwa.
- Utabiri wa viwavijeshi hufanyika ili kutambua uwepo wa viwavi jeshi katika maeneo ya uzalishaji kwa ajili ya maandalizi ya kudhibiti mlipuko wa visumbufu hivyo ili kuhakikisha usalama wa mazao.
- Udhibiti wa magugu vamizi Salvinia spp na gugu maji (water hyacinth) katika ziwa Victoria na vyanzo vingine vya maji kwa kutumia njia za kibaiolojia kwa kuzalisha wadudu kama vile mbawa kavu na utitiri.
3. Anuani:
TPHPA Kanda ya Ziwa S.L.P 1484, Mwanza Tanzania
4. Barua Pepe:
- Meneja: [mary.leina@tphpa.go.tz]
- Kanda: [mwanza@tphpa.go.tz]