Prof. Joseph C. Ndunguru

WASIFU
TPHPA inaongozwa na Prof. Joseph C. Ndunguru kama Mkurugenzi Mkuu, akisimamia utekelezaji wa majukumu ya mamlaka kwa kuzingatia Sheria, kanuni na pia uwajibikaji na matarajio ya wadau. Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ni taasisi ya umma yenye dhamana ya kusimamia afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu ili kuhakikisha usalama wa mazao ya kilimo, afya ya binadamu, na mazingira na hivyo kuimarisha biashara ya mazao ndani na nje ya nchi. Chini ya uongozi wa Prof. Ndunguru, mamlaka inaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa kisekta , kuboresha mifumo ya udhibiti wa viuatilifu, na kuhakikisha kwamba wakulima na wazalishaji wa mazao wanapata huduma bora na zenye tija kwa maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
TPHPA pia ina jukumu la kuimarisha mifumo ya udhibiti wa visumbufu vya mimea; kutoa mwongozo wa kitaalamu kwa wakulima; na kuweka taratibu za kuhakikisha matumizi salama ya viuatilifu. Kupitia mifumo madhubuti ya usimamizi, mamlaka hii inatekeleza mikakati ya kupunguza athari za visumbufu vya mimea katika uzalishaji na pia athari ya matumizi ya viuatilifu kwa afya ya walaji na mazingira.