MAFURIKO HANANG: TPHPA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
MAFURIKO HANANG: TPHPA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Disemba 14,2023 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru ameongoza kundi la Viongozi na Watumishi wa Mamlaka hiyo kutembelea na Kutoa Msaada kwa Waathirika wa Maafa ya Mafuriko Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara yaliyotokea Usiku wa kuamkia Disemba 3,2023 na kusababisha uharibifu wa Mali,Vifo na Majeruhi
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Prof. Ndunguru amesema kuwa Mamlaka hiyo imeguswa na tukio hilo hivyo imekuja kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha waathirika wa Mafuriko Mkoani hapo wanasaidiwa ili waweze kurudi katika hali zao za kawaida, aidha pia ametumia wasaa huo kutoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika tukio hilo huku akiwaombea waliopata majeraha kupona haraka na kurejea katika shughuli za kulijenga Taifa
Kupitia msaada huo Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imetoa vyakula na Vifaa vya wanafunzi kamavile Mchele tani 2, maharage tani 1, mafuta ya kula lita 200, unga wa ngano kilo 500, sabuni ya unga mifuko 10,madaftari kwaajili ya wanafunzi katoni 22, penseli dazeni 24,kalamu katoni 2,vifutio pisi 300
Akipokea Msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hanang Ndg. Francis Namaumbo kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, ameushukuru uongozi wa Mamlaka kwa Kuchukua hatua ya kwenda kuwatembelea na kuwapa msaada wahanga wa maafa hayo kwani kufanya hivyo kunazidi kuwapa faraja na kuwapunguzia makali ya Maisha.
Akizungumza kwaniaba ya Waathirika wa Mafuriko hayo ambao watanufaika na Msaada huo Victoroa Kimambo ameushukuru uongozi wa TPHPA na wafanyakazi wake kwa moyo waliouonyesha wa kuwasaidia katika kipindi kigumu huku akiwataka kuendelea kuwaombea ili warejee katika hali zao za kawaida