MHE. RAIS ATOA TUZO KWA TPHPA KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE KITAIFA MKOANI DODOMA.
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imepata heshima kubwa kwa kushinda tuzo na kushika nafasi ya pili katika kundi la wakala wa serikali,huduma na uzalishaji.Tuzo hii inatokana na mchango wa Mamlaka katika kukuza uzalishaji wa Mazao kwaajili ya Matumizi ya Ndani na Nje ya Nchi, kuimarisha Afya ya mazao, na kulinda mazingira.
Tuzo hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 8,2024 Wakati wa Kilele cha maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nane nane 2024) Kitaifa Mkoani Dodoma hapa Viwanja vya Nzuguni
Mamlaka imejizatiti katika kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu, pamoja na kuendeleza kutoa huduma za kuhakikisha Mazao bora yanazalishwa Nchini kwaajili ya Biashara. Ushindi huu unadhihirisha dhamira ya Mamlaka katika kuhakikisha usalama wa chakula na kuimarisha sekta ya kilimo.