Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

MWIGULU AIPONGEZA TPHPA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WAKULIMA NCHINI

Imewekwa: 03 Aug, 2026
MWIGULU AIPONGEZA TPHPA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WAKULIMA NCHINI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigułu Lameck Nchemba (Mb), ameiipongeza Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa kutoa huduma bora kwa wakulima. Pongezi hizo amezitoa leo mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya 33 ya Siku ya Wakulima Nanenane 2026 yaliyofanyika viwanja vya Nzuguni, Dodoma.

Akiongozana na Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na mawaziri kutoka wizara nyingine, Dkt. Nchemba alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Prof. Joseph Ndunguru, ambaye amemweleza mafanikio makubwa yaliyofanywa na Mamlaka. Prof. Ndunguru alimjulisha kuwa TPHPA imeimarisha jitihada za udhibiti wa baa la panya, kutoa elimu ya matumizi salama ya viuatilifu na kuhakikisha afya ya mimea inalindwa ili kuongeza tija kwa wakulima.

Dkt. Nchemba amesema utendaji wa TPHPA ni mfano mzuri wa utekelezaji wa kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu "Tambúa Soko; Ongeza Tija Kutekeleza DIRA 2050". Ameelekeza Mamlaka kuendelea kuboresha huduma na kufika kwa wakulima zaidi ili kulinda mazao na kuimarisha usalama wa chakula nchini.