Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

BODI YA PAMBA NA TPHPA YAPIGILIA NONDO SUMU ZISIZO NA LESENI.

Imewekwa: 30 May, 2024
BODI YA PAMBA NA TPHPA YAPIGILIA NONDO SUMU ZISIZO NA LESENI.

BODI YA PAMBA NA TPHPA YAPIGILIA NONDO SUMU ZISIZO NA LESENI.

 

Bodi ya Pamba Tanzania imefanya ziara Makao Makuu ya Mamlaka ya Afya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) mkoani Arusha Mei 28, 2024 ambapo ilikuwa imeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Mhe. Christopher Gachuma na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Mhe. Marco Mtunga.

 

Ziara hiyo ilitanguliwa na mkutano kati ya Bodi ya Pamba na Menejimenti ya wafanyakazi ya TPHPA ambapo hoja kuu ilikuwa ni kuhusu viuatilifu visivyo na leseni vinavyotumiwa na wakulima wa pamba na hivyo kusababisha kudorora kwa zao hilo na hivyo kusababishia wakulima hasara.

 

Akitoa hoja hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Mhe. Marco Mtunga alisema kuwa wamekuwa wakibaini viuatilifu visivyo na leseni kutoka TPHPA vikitumiwa mashambani mwa wakulima wa Pamba na kuzua malalamiko makubwa kutoka kwa wakulima hao na hivyo kuitaka Mamlaka hiyo kushirikiana nao katika kuondoa kero hiyo kwani inasababisha zao hilo la Pamba kukosa soko kwa kuwa na kiwango kisichoridhisha.

 

Aidha mjumbe wa Bodi na Balozi wa Pamba Tanzania Mhe. Aggrey Mwanri aliongezea kwa kuelezea kuwa sumu hizo zisizo na leseni zinaathiri mazingira pamoja na wakulima na hivyo kusisitiza wakulima kupewa Elimu ya matumizi Sahihi na Salama ya viuatilifu ili kuepusha madhara makubwa yanayosababishwa na viuatilifu kwa mkulima na mazingira kwa ujumla.

 

Akizungumza kwa upande wa Mamlaka, Kaimu Meneja kitengo cha Teknolojia ya VInyunyizi Dkt. Magret Francis ameeleza ni kwa kiasi gani wamekuwa wakitoa Elimu ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu kwa wakulima ikiwa ni shughuli endelevu inayofanyika nchi nzima kwa kuwapeleka wataalamu maeneo mbalimbali nchini kueneza Elimu hiyo hususani kwa wakulima na Wafanyabiashara wa Viuatilifu.

 

Baada ya Mkutano huo uliojadili mambo mbalimbali kuhusu zao la Pamba na uboreshaji wake, Bodi ya Pamba ilipata nafasi ya kutembelea maabara zilizopo Mamlaka ya Afya ya Mimea ambazo huwa zinatumiwa katika kutekeleza majukuma makuu ya Taasisi hiyo ikiwemo za kupima na kuhakiki viuatilifu vinavyotaka kusajiliwa nchini.