Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

MKURUGENZI MKUU TPHPA AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKAGUZI WA VIUATILIFU,ABAINISHA MAFANIKIO YATAKAYOPATIKANA ,ATAJA MWAKA 2024 KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA KWA MAMLAKA

Imewekwa: 09 Jan, 2024
MKURUGENZI MKUU TPHPA AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKAGUZI WA VIUATILIFU,ABAINISHA MAFANIKIO YATAKAYOPATIKANA ,ATAJA MWAKA 2024 KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA KWA MAMLAKA

MKURUGENZI MKUU TPHPA AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKAGUZI WA VIUATILIFU,ABAINISHA MAFANIKIO YATAKAYOPATIKANA ,ATAJA MWAKA 2024 KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA KWA MAMLAKA

 

Hayo yamebainishwa Januari 08, 2024 wakati Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu(TPHPA) Prof.Joseph Ndunguru akifungua mafunzo ya siku 5 kwa wakaguzi wa viuatilifu    kutoka TPHPA katika ukumbi wa PANAMA Hotel jijini Moshi ambapo Mkurugenzi huyo amebainisha manufaa ya mafunzo hayo kwa nchi na kwa Mamlaka.


Akiongea mara baada ya kufungua mafunzo amesema mafunzo kwa Wataalam wa TPHPA katika maeneo mbalimbali ni moja ya  jukumu kubwa la Mamlaka ili kuhakikisha lengo la mamlaka kuhakikisha afya ya mimea linafikiwa .

Akibainisha faida ya mafunzo hayo amesema kuwa wataalam hao wanajengewa uwezo ili waweze kufanya majukumu yao ya ukaguzi kwa weledi jambo ambalo litapelekea  kulinda afya ya binadamu,mimea na mazingira.

Pamoja na hayo mafunzo  yatapelekea kuongeza tija katika uzalishaji kwani ukaguzi utakapofanyika kitaalam na kuzuia yale yote ambayo yangepelekea kuharibu uzalishaji matokeo yake ni kuongezeka tija katika mazao ambayo itapelekea uboreshwaji wa masoko ya mazao kwa kiwango kinachohitajika hata kwa masoko ya kimataifa,

Aidha kupungua kwa Visumbufu katika mimea kwani ukaguzi unasaidia kupata viuatilifu sahihi vyenye tija kwa mimea kwani 
ukaguzi hupelekea kuondosha viuatilifu bandia sokoni.


Akizungumzia vifaa vya utekelezaji amesema TPHPA imesambaza vifaa vya kutosha katika kanda zake 7 na vituo vyake vyote ikiwepo magari na pikipiki kwa ajili ya kurahisisha ukaguzi vituoni na mipakani.


Vilevile amegusia matarajio yake kwa mwaka 2024 akihusisha na mafunzo haya amesema ana matumaini makubwa utekelezaji unaenda kuleta mafanikio makubwa kwa mwaka huu wa 2024 kwani Mamlaka imejipanga kuona kwamba hakuna litakalokwama katika kutekeleza majukumu yake ikiwepo  kuhakikisha kuongezeka kwa pato la taifa kutokana na biashara ya mazao nje ya nchi kwa kuhakikisha viwango vya ubora wa mazao vinafikiwa ikiwepo ubora na usafi wa mazao.


Pia amewashukuru Umoja wa Ulaya kupitia  FAO kwa kudhamini mafunzo hayo kwa wakaguzi wataalam wa TPHPA.


Akitoa wito kwa washiriki Prof.Ndunguru amewataka kuzingatia maelekezo wanayofundishwa ili malengo yanayotarajiwa yakafikiwe.