Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

Mkurugenzi wa TPHPA Afungua Mafunzo ya 59 ya Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wafanyabiashara na Wakulima.

Imewekwa: 06 Nov, 2023
Mkurugenzi wa TPHPA Afungua Mafunzo ya 59 ya Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wafanyabiashara na Wakulima.

MKURUGENZI WA TPHPA AFUNGUA MAFUNZO YA 59 YA MATUMIZI SAHIHI YA VIUATILIFU KWA WAFANYABIASHARA NA WAKULIMA, AZUNGUMZIA KUFUNGUKA MASOKO YA KIMATAIFA

Novemba 6, 2023 Mkurugenzi wa TPHPA Prof.Joseph Ndunguru amefungua mafunzo ya 59 ya matumizi sahihi ya Viuatilifu yanayotolewa na Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu TPHPA kwa wafanyabiashara na wakulima yenye lengo la kutoa elimu ya Matumizi sahihi ya Viuatilifu ili kuepuka madhara kwa binadamu na mazingira yanayotokana na Matumizi yasiyo sahihi .

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Prof.Ndunguru amesema moja ya jukumu kubwa ya TPHPA ni kudhibiti matumizi ,utengenezaji na usambazaji wa Viuatilifu,kwa hiyo kwa kutoa mafunzo hayo ni moja ya utekelezaji wa shughuli za Mamlaka zenye lengo la kutoa elimu itakayosaidia  kupunguza athari kwa jamii na mazingira  kutokana na  matumizi yasiyo sahihi ya Viuatilifu.

Sambamba na hilo amesema kuwa matumizi sahihi ya Viuatilifu ni muhimu kwani pamoja na kupelekea mimea kuwa na Afya na kuepuka athari mbalimbali lakini pia inasaidia katika kufungua masoko ya nje Kwa bidhaa zetu na hata kuongeza pato la tafa na faida Kwa mkulima ,kwani utakapomtumia Viuatilifu kwa usahihi itasaidia Kupunguza uwezekano wa kuwepo Kwa mabaki ya simu katika mazao ambayo pia yanatarajiwa kuuzwa nje ya nchi na kupelekea kukidhi matakwa na vigezo vya kimataifa katika mazao kwani upimaji hufanyika ili mazao kuweza kukubalika na kuuzwa nje ya nchi.

Akitoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo amewataka kuzingatia kwa makini mafunzo hayo na kuwataka kutokusita wakati wowote kuwasiliana na Mamlaka pale wanapohitaji msaada au maoni Mamlaka ipo tayari kusaidia."Na hatutaishia hapo tutakuja kuwatembelea katika biashara zenu na mashamba yenu ili kuona jinsi mnavyotumia mafunzo hata kwa vitendo lakini pia kupata mrejesho kutoka kwenu juu ya kile mlichofundishwa."alisema prof Ndunguru

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Afya ya Mimea  wa TPHPA  Dkt.Benignus Ngowi amewataka washiriki hao kurudi tofauti na walivyokuja katika uelewa wa namna bora ya matumizi ya Viuatilifu na wakaitumie elimu hiyo Kwa manufaa yao na jamii Kwa ujumla.

Aidha mwakilishi wa Mratibu wa mafunzo ndg.Laurence Mapunda amebainisha masuala mada mbalimbali mbalimbali zitakazofundishwa kwa washiriki hao ikiwa ni pamoja na utambuzi wa visumbufu,matumizi sahihi ya Viuatilifu, umuhimu wa kufuata taratibu ili kupata kibali cha kuanza biashara za Viuatilifu,aina za biashara za viuatilifu.n.k

Akitoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kupata mafunzo haya msimamizi huyo amesema utafiti unaonyesha kuwa wakulima wengi wanapata maelekezo ya matumizi ya Viuatilifu kutoka kwa wafanyabiashara wakati wanapoenda kununua katika maduka yao hivyo ni vyema wakajitokeza kwa wingi pale mafunzo haya yanapotangazwa ili waweze kuhudhuria na kutoa maelekezo sahihi kwa wateja wao.

TPHPA imekuwa ikitoa mafunzo haya kila wakati kwa wafanyabiashara na wakulima Tanzania ambapo matangazo hutolewa kupitia mitandao ya kijamii ya mamlaka ya Instagram na tovuti tphpa_tz na YouTube TPHPA HABARI TV