Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

WAZIRI WA NCHI WA UGATUZI NA MASUALA YA MKOA NCHINI ZIMBABWE ATEMBELEA BANDA LA TPHPA

Imewekwa: 07 Jul, 2024
WAZIRI WA NCHI WA UGATUZI NA MASUALA YA MKOA NCHINI ZIMBABWE ATEMBELEA BANDA LA TPHPA

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeendelea kuwa kivutio katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama (Saba Saba) yaliyoanza Juni 28,2024 na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa nchi ya Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi Julai 3. 2024 

hukuyakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Tanzania mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji"  ikilenga kuonesha Dunia kubwa serikali ya awamu ya sita ipo tayari  na inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Ndani na nje ya nchi kufanya biashara na kuwekeza katika  sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo sekta ya Viwanda,kilimo,teknolojia,uwekezaji na Utalii.

Kutokana na huduma mbalimbali Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) inazozitoa ni elimu hususani fursa za biashara za mazao, Mhe. Ruvai Ezira, Waziri wa Nchi wa Ugatuzi na Masuala ya Mkoa nchini Zimbabwe, Julai 6, 2024 ametembelea banda la Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) pamoja na mambo mengine amepongeza shughuli mamlaka inazozifanya za hususani kuhakikisha inakagua na kuhakikisha usalama wa mazao ya Tanzania yanayouzwa nje ya nchi.