Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

TPHPA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA AFYA YA MIMEA

Imewekwa: 17 May, 2024
TPHPA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA AFYA YA MIMEA

 

TPHPA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA AFYA YA MIMEA

 

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea ambapo yalitanguliwa na maonesho ya bidhaa kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwepo wadau wa kilimo na wafanyabiashara wa viuatilifu kwa siku zote tatu hadi kufikia kilele Leo 12 Mei 2024.

Akizungumza mgeni rasmi Bi Hilda Kinanga Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Kilimo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg.Gerald Mweli ameupongeza uongozi wa TPHPA pamoja na Wafanyakazi wote kwa juhudi katika  kuchapa kazi .

Kwa namna ya pekee ameonyeshwa kuridhishwa na jinsi TPHPA inavyojikita katika kutatua changamoto za Wakulima katika kudhibiti ndege waharibifu lakini pia kuhakikisha wakulima wanapewa elimu ya kutosha katika matumizi sahihi ya viuatilifu ili kuleta tija katika kilimo na kuwaongezea kipato.

Aidha ameishauri TPHPA kugawa mbegu za asili kwa wakulima ambazo zina tija Sana katika kilimo kulingana na ubora wake,"niwapongeze kwa utunzaji wa mbegu za asili lakini pia itakuwa vyema iwapo mtazigawa baadhi kwa wakulima waweze kunufaika nazo "alisema bi Hilda Kinanga.

Aidha amewahakikishia wadau na wajasiriamali waliokuwa wakionesha maonesho katika viwanja hivyo kuwa Serikali ipo panojabnao na  inatambua kazi wanayofanya  na bega kwa bega kutatua changamoto zao mbalimbali.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPHPA Prof. Andrew Temu ameishukuru serikali kwa jinsi inavyounga mkono juhudi za TPHPA na kuomba izidi kuunga mkono na  kushirikiana ili kufikia malengo yatakayoleta tija kwa wakulima.

Pamoja na hayo Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof.Joseph Ndunguru amefanya wasilisho la zao la Muhogo katika hafla hiyo lililokuwa na lengo la kuonesha umuhimu wa afya ya mimea unavyohusika moja kwa moja katika kuinua sekta hii ya kilimo na kubadilisha maisha ya Mkulima kwa kumuongezea kipato chake.Ambapo wasilisho Hilo limeonesha jinsi magonjwa ya Muhogo yalivyotambuliwa na kudhibitiwa kulikopelekea kuleta tija kwa Mkulima.