Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania

lbl_iso_certified

TPHPA yaadhimisha Siku ya Afya ya Mimea Dunia Jijini Arusha

Imewekwa: 14 Oct, 2023
TPHPA yaadhimisha Siku ya Afya ya Mimea Dunia Jijini Arusha

Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeendelea kuweka juhudi katika kulinda afya ya mimea kwa kuhakikisha wanaofanya kaguzi katika shena za vipando vinavyoingia nchini ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wakulima na maafisa ugani pamoja na kufanya ukaguzi wa viuatilifu sokoni ili kuliepusha taifa na upungufu wa chakula.

 

Hayo yalisema na kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Profesa Joseph Ndunguru wakati akiongea na waandishi wa habari katika kuadhimisha siku ya afya ya mimea Duniani ambapo alisema kuwa afya mimea inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo visumbufu kwa maana ya wadudu na magonjwa pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayofanya kuwepo kwa ukame hali inayopelekea kupungua kwa chakula na kuharibika kwa hewa safi.

 

“Asilimia 80 ya chakula inatokana na mimea lakini pia asilimia 98 ya oxygen inatokana na mimea na katika kuadhimisha siku hii mwaka huu kauli mbiu yetu ni Afya ya mimea kwaajili ya kupunguza umasikini, njaa na kulinda mazingira ili kukuza uchumi wa nchi zetu, na ili kuweza kufikia malengo haya ni muhimu kutunza afya ya mimea kwa kuwa na uthibiti ulio mahiri utakaoleta tija,” Alisema profesa Ndunguru.