TPHPA imeshinda tuzo ya mshindi wa kwanza katika katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imetwaa tuzo ya mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, leo Oktoba 16, 2024, katika viwanja vya CCM, Bukoba. Maonesho haya yalianza tarehe 10 Oktoba 2024.
Tuzo hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatma Mwassa.
Tuzo hii ina maana kubwa, kwani inaashiria kutambuliwa kwa juhudi za TPHPA katika kuimarisha usalama wa chakula na afya ya mimea nchini. Inadhihirisha umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za umma katika kukuza kilimo endelevu na lishe bora kwa jamii. Pia, inahamasisha uelewa wa umuhimu wa chakula katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na inatoa mwito kwa jamii kuwekeza katika lishe bora kwa ustawi wa vizazi vijavyo.