TPHPA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS, YAUNGANA NA TBC KUPANDA MITI ZAIDI YA 300
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, za utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kuungana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupanda miti zaidi ya 300 katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Arusha, Oktoba 27, 2026, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya 27 ya Kijani.
Zoezi hilo limeongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Prof. Joseph C. Ndunguru, akiungana na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo pamoja na TBC katika kuhamasisha jamii kushiriki shughuli za upandaji miti na utunzaji wa mazingira. Upandaji huo unalenga kuboresha mazingira, kuongeza uoto wa miti na kuimarisha uelewa kuhusu umuhimu wa miti katika kuhifadhi bayoanuai na kulinda mifumo ya ikolojia.